UGANDA

Serikali ya DRC yawatuhumu waasi wa M 23 kutekeleza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetuhumu  waasi wa M 23  kutekeleza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo .

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo kati ya wajumbe wa serikali na waasi yanaedelea jijini Kampala nchini Uganda huku kila upande ukivutia upande wake na kulaumiana.

Kiongozi wa ujumbe wa serikali Waziri wa mambo ya nje Raymond Tshibanda amewatuhumu waasi hao kwa kutekeleza mauaji, ubakaji, wizi na kuwatesa raia wa Mashariki mwa nchi hiyo.

Aidha, serikali ya Kinshasa inasema ushahidi wa kutisha kuwa waasi hao wametekeleza visa hivyo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ushahidi ambao pia wanasema Jumuiya ya Kimataifa unao.

Naye mwakilishi wa waasi wa M 23 Francois Ruchogoza hakujibu tuhma hizo za serikali dhidi yao lakini hapo awali aliituhumu serikali ya Kinshasa kwa ubaguzi wa watu wenye asili ya Kinyarwanda Mashariki mwa nci hiyo.

Msuluhishi Mkuu wa mauzngumzo hayo ya amani Waziri wa Ulinzi Crispus Kiyonga, anasema ana matumaini ya kuwa mazungumzo hayo yatazaa matunda na suluhu litapatikana ili amani ipatikane Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.