MISRI

Kura za kukubali au kukataa rasimu ya katiba mpya ya Misri zaendelea kuhesabiwa

Zoezi la kuhesabu kura za maoni zilizopigwa jana jumamosi kukubali ama kukataa rasimu ya katiba mpya ya Misri linaendelea nchini humo licha ya kutokuwa na maelewano baina ya wapinzani na wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood cha rais wa nchi hiyo Mohamed Mursi.

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Mursi wanadai kuwa kura za awali zinaonyesha asilimia 70 ya wapiga kura wameunga mkono rasimu hiyo wakati wapinzani wamekanusha madai hayo na kueleza kuwa asilimia 66 ya wapiga kura wamekataa kuunga mkono rasimu hiyo.

Matokeo kamili ya zoezi hilo yatatolewa baada ya kukamilika kwa awamu ya pili ya upigaji wa kura ambao utafanyika jumamosi ijayo disemba 22.

Wachambuzi wa siasa za nchi hiyo wanaona matokeo ya awamu ya kwanza huenda yakawa na ushawishi katika upigaji kura wa awamu ya pili.