TANZANIA-MALAWI

Joachim Chissano kupelekewa ombi la kuwa msuluhishi wa mzozo wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi

(Photo by HB Meeks/Tell Us Detroit)

Malawi na Tanzania wanatarajia kumwomba aliyekuwa Rais wa Msumbiji Joachim Chissano kuwa msuluhishi wa mgogoro wa Ziwa Nyasa suala ambalo muafaka wake ulikwama hapo awali baada ya Malawi kujitoa katika mazungumzo wakiishutumu Tanzania kutoa ramani nyingine tofauti inayoonesha mipaka ya Ziwa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Msumbiji Ephraim Chiume ujumbe wa Tanzania na Malawi utafika nchini Msumbiji siku ya kesho tarehe 20 mwezi disemba mwaka 2012 kuwasilisha ombi hilo.

Chiume amebainisha kuwa hatua hiyo inakuja baada ya wao kushindwa kuafikiana na hivyo wanaimani kuwa mazungumzo yataenda vizuri chini ya kiongozi huyo ambaye pia amewahi kuongoza jumuiya ya umoja wa nchi za kusini mwa Afrika SADC.

Wachambuzi wa maswala ya mizozo wanaona kuwa huenda kiongozi huyo akawa kiungo muhimu katika utatuzi wa mzozo huo kutokana na weledi wake katika maswala yahusuyo nchi za kusini mwa bara la Afrika.

Nchi hizi mbili zimekuwa katika mzozo wa Ziwa Nyasa ambapo Malawi inadai inahaki ya kumiliki eneo zima la ziwa wakati Tanzania inaendelea kushikilia msimamo wake wa kumiliki nusu ya ziwa hilo kama mpaka rasmi.

Mzozo wa mpaka katika Ziwa Nyasa uliibuka baada ya serikali ya Malawi kutoa kibali kwa wataalam kutoka nchini Uingereza kufanya utafiti wa mafuta katika Ziwa hilo karibu na mpaka wa Tanzania.