AFRIKA KUSINI

Nelson Mandela arejea nyumbani baada ya kupata nafuu

Rais wa kwanza Mzalendo nchini Afrika Kusini Nelson Mandela ameruhusiwa kutoka hospital baada ya kupatiwa matibabu kwa karibu majumatatu kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya mapafu.

Matangazo ya kibiashara

Nelson Mandela Madhiba mwenye umri wa miaka tisini na minne kwa sasa ameruhusiwa kutoka Hospital baada ya Jopo la Madaktari lililokuwa linamshughulikiwa kuridhishwa na hali yake ya sasa.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ndiye ambaye ametangaza kuruhusiwa kutoka Hospital ambako madakatari wamesema ataendelea kupata matibabu yakawaida akiwa nyumbani baada ya hali yake kurejea kama awali.

Mandela baada ya kuruhiswa kutoka Hospital moja kwa moja amepelekwa kijijini kwake ambako anaishi huko Qunu ambapo wananchi wa Taifa hilo wamekiri kuridhishwa na hatua ya Kiongozi wao wa zamani kutoka Hospital.

Maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini walishikwa na hofu kuu baada ya Mandela kupelekwa Hospital takaribani majuma matatu yaliyopita kutokana na kukabiliwa na maradhi ya mapafu.