Gabon

Waasi wa Seleka kuanza mazungumzo na Serikali ya Bozize kesho, wasisitiza Rais Bozize Kuondoka madarakani

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Froncois Bozize
Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Froncois Bozize

Waasi wa nchini Afrika ya kati wamerejea madai yao kuwa makubaliano yoyote ya kuleta amani yanayotarajiwa kuanza hapo kesho lazima yaambatane na kuondoka madarakani kwa Rais wa Taifa hilo, Froncois Bozize.

Matangazo ya kibiashara

Jumuia ya Nchi za Afrika ya kati CEEAC ina matumaini kuratibu mazungumzo hayo kati ya waasi na Rais Bozize jijini Libreville nchini Gabon ili kuweza kumaliza mzozo nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Hata hivyo wasiwasi uliopo ni kuwa mazungumzo hayo huenda yakaingia dosari kuwa kuwa Waasi wamekuwa wakisisitiza kuwa Rais Bozize aliyeingia madarakani mwaka 2003 ni lazima ajiuzulu shinikizo ambalo Bozize hakubaliani nalo.

Wawakilishi wa Bozize hii leo wameelekea Gabon huku Rais akitarajiwa kuelekea huko mara mazungumzo yatakapoanza.

Katika mazungumzo hayo, Ujumbe wa Serikali ya Rais Bozize utatoa mapendekezo juu ya mabadiliko ndani ya jeshi, mipango ya maendeleo ya kiuchumi na Tratibu za uchaguzi.