Mali

Wanajeshi wa Mali wapambana na Wanamgambo wa kiislamu kaskazini mwa nchi hiyo

Viongozi wa Kundi la Ansar Dine na MNLA  Wanaodhibiti eneo la Kaskazini mwa Mali
Viongozi wa Kundi la Ansar Dine na MNLA Wanaodhibiti eneo la Kaskazini mwa Mali Reuters

Wanajeshi wa Serikali ya Mali wamekabiliana na waasi wa kiislamu wanaoshikilia maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo katika kile kinachoelezwa waasi hao kujaribu kusonga mbele kuelekea kaskazini zaidi. 

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo ya hivi karibuni yanajiri ikiwa ni saa 48 toka majeshi ya magharibi mwa Afrika yajaribu kutekeleza operesheni kwenye mji wa Konna kujaribu kuwasambaratisha waasi hao.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia mapigano hayo wamesema kuwa kwa mara ya kwanza yamehusisha silaha nzito ukilinganisha na makabiliano yaliyotokea juma moja lililopita.

Vikosi vya Serikali ya mali vimeanza operesehni kujaribu kurejesha maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo kwenye himaya yao.

Mapambano haya yamekuja baada ya Majeshi ya NATO kusema kuwa hayajaombwa kusaidia Vikosi vya Afrika kulirejesha eneo la kaskazini mwa Mali mikononi mwa Mamlaka ya nchi hiyo.