TANZANIA-UGANDA-TUNISIA

Emmanuel Okwi wa Simba ajiunga na Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa mkataba mnono

RFI

Mshambuliaji wa Klabu ya Simba ya Tanzania Emmanuel Okwi amejiunga na Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa mkataba wa kitita cha dola 300,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 450.

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo wa Okwi mwenye asili ya Uganda unaweka historia kwa mchezaji kutoka klabu ya Tanzania kubeba kitita kama hicho.
 

Okwi ambaye alijiunga na Simba mwaka 2010 akitokea klabu ya SC Villa ya Uganda alifaulu vipimo vyake vya mwanzoni mwa juma hili na atakuwa akivuna kitita cha dola 15,000 za kimarekani kila mwezi.

Uongozi wa Simba kupitia kwa msemaji wake Ezekiel Kamwaga amesema kuwa timu hizo zimemalizana kuhusu suala la mchezaji na Simba na kusema kuwa huo ni mkataba mnono ambao Simba isiweza kuukwepa.
 

Kamwaga amesema kuwa fedha ambazo zimetokana na mauzo ya mchezaji huyo zitatumika pamoja na mambo mengine kunua wachezaji wengine kupitia dirisha dogo.
 

Mchezaji Okwi mwenye umri wa miaka 21 aliisaidia klabu yale ya Simba kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Tanzania, Vodacom Premier League katika msimu wa 2011-12.
 

Pia aliisaidia Simba kufikia hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kombe la Kagame ikiwa ni pamoja kutwaa ngao ya hisani ya jamii baada ya klabu yake kushinda kwa bao 3-2 dhidi ya Azam FC.