SOMALIA-UFARANSA

Wanamgambo wa Al Shabab watishia kumuua afisa wa kijasusi wa Ufaransa Denis Allex

RFI

Wanamgambo wa Al-Shabab nchini Somalia wanasema watamuua afisa wa kijasusi raia wa Ufaransa Denis Allex, ambaye wamekuwa wakimzuia tangu mwaka 2009. Tangazo hilo la Al-Shabab linakuja siku mbili baada ya kutangaza kufariki kwa mmoja wa Makomandoo wa Ufaransa waliokuwa katika Oparesheni ya kumwokoa afisa huyo wa ujasusi.

Matangazo ya kibiashara

Al-Shabab wanasema wamefikia uamuzi huo kwa pamoja na uamuzi huo hautabadilishwa.

Hata hivyo taarifa kutoka kwa kundi hilo haijaeleza ikiwa Dennis Allex bado yuko hai au tayari amekwishauawa.

Serikali jijini Paris hata hivyo inasema kuwa haiamini kuwa afisaa wake bado ni mzima na wanashuku kuwa tayari ameshauawa na wanamgambo hao.

Denis Allex amevunja Historia kuwa mateka raia wa ufaransa ambaye amekuwa akizuiliwa kwa muda mrefu sana na wangambo wa Al-Shabab ambao wamekuwa wakisema juhudi za mawasiliano kati yao na Ufaransa zimekuwa zikigonga mwamba.

Kundi hili la kigaidini linalohushwa na Al -Qeda linasalia hatari kwa usalama katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati.