MALI

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS yaiomba UN msaada wa haraka kuisaida Mali

Rais wa Cote D'voire Alassane Ouattara,na mkuu wa sasa wa ECOWAS
Rais wa Cote D'voire Alassane Ouattara,na mkuu wa sasa wa ECOWAS thelondoneveningpost.com

Viongozi wa jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Magharibi mwa Africa ECOWAS wametoa wito wa msaada wa haraka kutoka kwa umoja wa mataifa kwa ajili ya jeshi lake kwenda kupambana na waasi wa Kiislam nchini Mali wakati rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa askari wake wataendlea kusalia nchini Mali kadri wanavyohitajika ili kumaliza ugaidi. 

Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa dharura wa Jumuiya hiyo ya (ECOWAS) pia imetoa wito kwa nchi wanachama na Chad, ambayo imeahidi askari 2,000, kutekeleza haraka ahadi zao kwa vitendo bila kusita.

Wanajeshi wa Afrika wapatao mia moja pekee kati ya kikosi cha wanajeshi 5800 kilichopangwa, ndio wamewasili nchini Mali hadi sasa ambapo Ufaransa imesema kuwa wanajeshi wa Ufaransa wapatao elfu mbili wako nchini Mali baada ya Paris kufanya shambulizi juma lililopita dhidi ya wanamgambo wa kiislam.