DRCongo-Afrika Kusini

Watu 19 raia wa DRCongo wakamatwa nchini Afrika Kusini kwa tuhuma za kujiandaa kwa mapinduzi ya serikali ya rais Kabila

Mahakama nchini Afrika kusini yathibitisha kuwa washukiwa kumi na tisa wenye asili ya jamuhuru ya kidemokrasia ya Congo DRC waliokamatwa jana Jumanne nchini humo, walikuwa na lengo la kupewa mafunzo maalum ya kijeshi kwa ajili ya kwenda kufanya mapinduzi ya serikali ya rais Joseph Kabila Kabange.

Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila
Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo nchini Afrika Kusini imesema hakuna ishara yoyote inayo onyesha uhusiano wa kundi hilo na kundila waasi wa M23 linalo pambana na serikali ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo huko mashariki mwa nchi hiyo tangu Mei mwaka 2012.

Msemaji wa mahakama Makhosini Nkosi, amesema, lengo hasa la kundi hilo ilikuwa ni kupewa mafunzo maalum ya kijeshi nchini humo kwa ajili ya kwenda kufanya mapinduzi ya serikali. Washukiwa hao walikamatwa na kikosi maalum cha polisi katika eneo lililoachawa kaskazini mwa nchi hiyo.

Msemaji huyo wa mahakama ameweka wazi kwamba washukiwa hao watafikishwa mahakamani kesho alhamisi kwa makosa ya kuvunja sheria za kijeshi na watasafirishwa nchini mwao baada ya kusikilizwa kwa kesi yao.

Kundi lingine la watu huenda wakakamatwa, lakini hata hivo hakuna raia hata mmoja wa Afrika Kunsini aliehusishwa na mpango huo wa uhaini.

Msemaji wa serikali ya DRCongo Lambert Mende amekiri kuwa wamepokea taarifa hiyo ya kukamatwa kwa watu 19 ambao waliakamtwa wakati walipokuwa wakijiandaa kwa mafunzo.

Takriban raia laki tatu wa DRCongo wanakadiriwa kueshi nchini Afrika Kusini ambao wengi wao ni wapinzani wa serikali ya Rais Joseph Kabila.