Wakili wa Uhuru Kenyatta katika kesi ya ICC asema atawakilisha ombi la kuachiwa huru mteja wake baada ya shahidi kudai kuwa alitowa ushaidi wa uongo

Wakili wa Naibu Waziri Mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia anawania urais nchini humo Steven Kay anataka Mahakama ya Kimataifa ya ICC kuachana na kesi inayomkabili mteja wake baada ya shahidi mmoja upande wa Mashtaka kudai kuwa alitoa ushahidi wa uongo.

Uhuru Kenyatta Mgombea urais nchini Kenya, na makam wake William Rutto
Uhuru Kenyatta Mgombea urais nchini Kenya, na makam wake William Rutto
Matangazo ya kibiashara

Wakili Kay anasema shahidi huyo alidanganya kuwa alikuwepo katika Mkutano katia ya Uhuru Kenyatta na kundi la Mungiki linalotuhumiwa kutekeleza mauaji dhidi ya wafuasi wa Waziri Mkuu Raila Odinga mjini Nakuru na Naivasha.

Hata hivyo wataalam wa sheria za kimataifa wansema kuwa ombi la wakili wa Uhuru haliwezi kuzaa matunda na lingeweza kufua dafu ikiwa lingewasilishwa na kiongozi wa Mashtaka.

Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta, William Ruto, Mwandishi wa Habari Joshua Sang, na aliyekuwa mtumishi wa umma Francis Muthaurna inatarajiwa kuanza tarehe 11 mwezi wa nne kwa tuhma za kuchochea na kufadhili machafuko ya baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 na kusababisha zaidi ya watu elfu moja kupoteza maisha.

Licha ya kukabiliw ana kesi hiyo Uhuru Kenyatta ambae anawania kiti cha Uchaguzi urais mkuu katika uchaguzi unatarajia kupigwa mwezi March mwaka huu nchini Kenya na mwezie William Ruto wanaendelea na kampeni za uchaguzi kuhakikisha wanafikia azma yao ya kuingia ikulu.