DRCongo-SADC

Viongozi wa SADC kukutana leo nchini Msumbiji kujadili suala la DRCongo

Rais wa msumbuji Armando Guebuza ameitisha kikao cha dharula cha viongozi wa jumuiya kicuhumi ya nchi za kusini mwa bara la Afrika SADC jiji Maputo Ijumaa hii, ili kujadili kuhusu hali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Viongozi wa Ikulu ya rais nchini Msumbuji wamesema kwamba mkutano huo utajadili kuhusu maendeleo ya kisiasa nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo bila hata hivo kutokwa muelezi zaidi.

Viongozi wa SADC katika moja ya vikao jijini Dar Es Salaam
Viongozi wa SADC katika moja ya vikao jijini Dar Es Salaam
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete kiongozi wa kamati ya Usalama na Ulinzi ya SADC na rais wa jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Joseph Kabila wametangaza kushiriki kikao hicho.

Wajumbe mkutanoni watajaribu kujadili kuhusu tofauti zolizopo katika SADC kuhusu kutumwa kwa vikosi vya kulinda amani mashariki mwa DRCongo, suala ambalo linaonekana kukwamisha kusaini makubaliano ya amani yalioitishwa na Umoja wa Mataifa.

Duru za kidiplomasia zinaarifu kuwa nchi tatu ambazo zipo tayari kutuma vikosi vyao huko mashariki mwa DRCongo, Afrika Kusini, Tanzania na Msumbuji zinataka kuwa huru katika uongozi na sio kuwa chiniya uongozi wa Umoja wa Mataifa.

Kikosi cha huduma za haraka chenye kuundwa na wanajeshi 2.500 ambacho Umoja wa Mataifa unataka kuunda kinatakiwa kuwa na uwezo wa kuingilia haraka iwezekanavyo, badala ya ilivyo kwa sasa na vikosi 17.000 vya operesheni ya Umoja wa Mataifa MONUSCO vikiwa na majeshi ya FARDC, lakini pia vikiwa pekeavyo vikijitegemea kwa uwezo maalum.

Jeshi la Congo FARDC linapambana tangu mwezi April 2012 na kundi la waasi wa M23, waasi ambao Umoja wa Mataifa unasema waungwa mkono na Rwanda na Uganda.

Mzungumzo ya amani yanaendelea huko Kampala Uganda baina ya wajumbe wa serikali na waasi wa m23