Ethiopia

Mataifa ya Ukanda wa Maziwa makuu yatia saini makubaliano ya amani ya Mashariki wa Congo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiwa mjini Adis Ababa nchini Ethiopia
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiwa mjini Adis Ababa nchini Ethiopia AFP / Maina

Viongozi kutoka Mataifa ya Maziwa Makuu wametia saini mkataba wa amani kuhusu usalama wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokarais ya Congo. 

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo ulitiwa saini jijini Adddis Ababa Ethiopia kati ya marais hao na Umoja wa Mataifa,huku UN ikiahidi kutuma vikosi vya majeshi kukabiliana na waasi Mashariki mwa nchi hiyo.

Nchi 11 za ukanda wa maziwa Makuu zikiwemo zile zinazoshutumiwa kuyaunga mkono makundi ya waasi walitia saini mkataba huo tukio lililoshuhudiwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon

Ban Ki Moon amesema kuwa ana matumaini kuwa makubaliano hayo yatasaidia kuleta amani Mashariki mwa DRC na kumaliza makabiliano kati ya waasi wa M 23 na serikali.

Baada ya kutia saini makubaliano hayo Balozi wa Marekani ndani ya Umoja wa mataifa, Susan Rice ameyaonya mataifa hayo kuheshimu Makubaliano hayo na kuacha kuunga mkono Uasi.
 

Mkataba huu umetiwa saini wakati waasi wa M 23 wakiendelea na mazungumzo na serikali jijini Kampala Uganda na hadi sasa suluhu bado halijapatikana.