Mali

Ukosefu wa usalama nchini Mali wasababisha Wanafunzi zaidi ya 700,000 kutokwenda Shule

Umoja wa Mataifa unasema kuwa ukosefu wa usalama Kaskazini mwa Mali umesababisha zaidi la wanafunzi laki saba kutoenda shule.

Wanajeshi wa Mali wakiendelea na Operesheni yao kaskazini mwa Mali
Wanajeshi wa Mali wakiendelea na Operesheni yao kaskazini mwa Mali REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Shirika la UNICEF linaloshughulika na maswala ya watoto katika Umoja huo liansema kuwa kufungwa kwa zaidi ya shule 100 kumesababisha wanafunzi kusalia nyumbani kwa hofu ya kuvamiwa na waasi wa kiislamu.
 

Shirika limesema kuwa walimu pia wameshindwa kurejea kaskazini mwa nchi hiyo na kuwa shule zilizopo kusini mwa Mali zimejaa kiasi cha kushindwa kumudu idadi kubwa ya wanafunzi kutoka Kaskazini.
 

Operesheni ya kupambana na makundi ya kiislamu nchini Mali imekuwa ikiendelea ili kulinusuru eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.