Kenya

Wakenya wafanya maandalizi ya Uchaguzi mkuu utakaofanyika Juma lijalo

Wagombea wa urais nchini Kenya
Wagombea wa urais nchini Kenya

Wagombea urais nchini Kenya kwa mara ya kwanza walikutana jana Jumapili wakati wa maombi ya kitaifa jijini Nairobi na kuhimiza amani nchini wakati wa uchaguzi Mkuu utaofanyika siku ya Jumatatu juma lijalo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati hayo yakijiri wakenya walishiriki katika upigaji kura wa majaribio kote nchini zoezi ambalo tume huru ya uchaguzi ilisema ilikuwa fursa ya kuwaonesha wakenya namna watakavyopiga kura.
 

Zoezi hilo lililoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC, linalenga kupunguza dosari za kuharibika kwa kura wakati wa uchaguzi ambapo Raia waishio katika kata zaidi ya 1000 nchini humo
 

zoezi hilo limepokelewa vizuri na Raia nchini humo wakikiri kupata manufaa ya kufahamu namna ya kufuata taratibu za kupiga kura kwenye uchaguzi ujao, huku wengine wakisema kuwa taratibu za kufuata zimekuwa zikiwakanganya.
 

Zimesalia siku sita Raia wa nchi hiyo kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba kupiga kura ambapo uchaguzi huo utafanyika juma lijalo.