Mali

Wanajeshi wa Mali washutumiwa kujihusisha na vitendo vya ukiukaji wa Haki za Binaadam

Wanajeshi wa Mali wakiendelea na Operesheni yao kaskazini mwa Mali
Wanajeshi wa Mali wakiendelea na Operesheni yao kaskazini mwa Mali REUTERS/Joe Penney

Wanajeshi wa Mali wanaopambana na Waasi wa Kiislamu Kaskazini mwa nchi hiyo wameamriwa kurudi nyuma katika oparesheni zao baada ya kutuhumiwa kuhusika na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi la Mali Modibo Naman Traore amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya Raia katika mji wa Timbuktu kulalamika kuwa walikuwa wanadhalalishwa na wanajeshi hao suala ambalo pia limelalamikiwa pia na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Majeshi ya Mali na Ufaransa yamekuwa katika mstari wa mbele kupambana na waasi Kaskazini mwa nchi hiyo na wamefanikiwa kuwafurusha kutoka katika miji hiyo.

Majeshi hayo yaliingia nchini Mali tarehe 11 mwezi Januari baada ya makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali yaliyokuwa yanadhibiti eneo lakaskazini mwa Mali kuanza kujisogeza maeneo ya kusini mwa nchi hiyo na kutishia kuukaribia Mji mkuu wa Mali.