Sudani

Zaidi ya wafuasi 500 ya jamii ya Waaarabu wauawa huko jimboni Darfur nchini Sudani

Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiiri
Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiiri UN Photo/Isaac Billy

Zaidi ya wafuasi 500 wa Kabila Jamii ya Waarabu katika jimbo lenye machafuko la Darfur wameuawa na wengine takriban 900 wamejeruhiwa katika Majuma saba ya mapigano.

Matangazo ya kibiashara

Idadi hiyo imeelezwa kuwa kubwa zaidi kuliko ile iliyotolewa awali baada yakutokea mapigano kati ya watu wa Jamii ya Rezeigat na Mahasimu wake wa kabila la Beni Hussein.
 

Walinda amani nchini Sudani waliwanusuru Raia 37 waliokuwa wamejeruhiwa, ili kuwapatia matibabu mjini El Fasher, Majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID yameeleza.
 

Katika shambulio la siku ya jumamosi, Wakazi wa mjini El Sireaf wamesema kuwa wanamgambo wa Jamii ya Rezeigat walifanya mashambulizi kwa risasi,Roketi na maguruneti wakifanya uharibifu wa nyumba na kusababisha watu zaidi ya 50 kupoteza maisha.
 

Hii leo Darfur inatimiza miaka 10 tangu Waasi kutoka jamii isiyo ya Waarabu kuanza kushambulia Serikali yenye jamii kubwa ya Waarabu, hata hivyo imeelezwwa kuwa sura ya machafuko hivi sasa imebadilika na kuwa Machafuko ya kikabila kama yale yanayofanyika mjini Jebel Amir.