Misri

Chama cha upinzani NSF chatangaza kugomea uchaguzi wa Mwezi Aprili

Rais wa Misri, Mohamed Morsi
Rais wa Misri, Mohamed Morsi AFP PHOTO/FAYEZ NURELDINE

Chama cha upinzani nchini Misri kimetangaza kujiondoa katika uchaguzi utakaofanyika Mwezi Aprili wakishuku kuwa uchaguzi huo hautaendeshwa kwa uwazi na kukataa wito wa kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo, Mohamed Morsi.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na kuwepo kwa msuguano kati ya Chama tawala cha Kiislamu na upinzani Rais wa Marekani, Barack Obama amemwambia Rais Morsi kuwa ana wajibu wa kulinda Demokrasia iliyopatikana kutokana na mapinduzi ya Mwaka 2011.
 

Amezitaka pande zote mbili nchini Misri kukubaliana na ili kujadili mustakabali wa kisiasa nchini humo.
 

Chama cha National Salvation Front (NSF) kimesema kitasusia uchaguzi huo mpaka pale kutakapokuwa na Sheria itakayosimamia mchakato wa uchaguzi wa uwazi .
Uamuzi huo umekuja baada ya madai ya Chama hicho ya kutaka kuundwa kwa Serikali mpya kutupiliwa mbali.
 

Chama cha NSF kiliandaa Maandamano makubwa mwezi Novemba na Disemba dhidi ya Morsi ambapo wandamanaji walidai Kiongozi huyu amejilimbikizia madaraka.