Marekani

Ufaransa kutoa Mapendekezo ya kupelekwa kwa vikosi vya UN vya kulinda amani nchini Mali mwezi Aprili

Ufransa ambayo Majeshi yake yanapambana na wanamgambo wa kiislamu nchini Mali hawatatoa pendekezo rasmi juu ya kupelekwa kwa vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani mpaka itakapofika mwezi Aprili, Balozi wa Ufaransa ndani ya Umoja wa Mataifa ameeleza. 

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande AFP PHOTO / POOL / ALEXANDER NEMENOV
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa ilipeleka Vikosi vya kijeshi nchini Mali, mwezi Januari ili kupambana na Makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali waliokuwa wamedhibiti eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.
 

Mjumbe wa Ufaransa ndani ya Umoja wa Mataifa, Gerard Araud amesema Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa lilikubaliana kumwandikia Barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon wakimtaka kusaidia kutafuta namna ya kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani.
 

Ufaransa imetangaza kuanza kuondoa Vikosi vyake vya Wanajeshi 4,000 kutoka nchini Mali kuanzia mwezi March.
 

Hata hivyo ikiwa maazimio yatafanyika Mwezi Aprili, kwa kawaida huchukua mpaka Miezi mitatu kwa Umoja wa Mataifa kutekeleza maazimio hayo.
 

Vikosi vya Afrika vimejikusanya tayari nchini Mali ambavyo vitashirikiana na vya Umoja wa Mataifa hata hivyo walinda amani hawa hawatakuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya Wanamgambo hao kama Vikosi vya Ufaransa na Chad vilivyofanya.