Sudani

Khartoum kupeleka Mamia ya Wanajeshi wake katika eneo lenye Mzozo la Jimbo la Blue Nile

Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiiri
Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiiri UN Photo/Isaac Billy

Sudan inapeleka Mamia ya Wanajeshi wake katika jimbo lenye mzozo la Blue Nile, baada ya kutolewa Ripoti kuwa kumekuwepo na mapigano kati ya Majeshi ya nchi hiyo na Waasi katika mji huo.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imelenga kuimarisha usalama katika Jimbo la Blue Nile na kuwasambaratisha Waasi.

Waasi wa SPLM-N Mwishoni mwa Juma lililopita walidai kuwa wameingia katika
eneo la kusini magharibi mwa Jimbo hilo madai yaliyokanwa na Msemaji wa Majeshi ya Sudan Sawarmi Khaled ambaye alisema kuwa madai hayo si ya kweli.
 

Serikali ya Khartoum inaishutumu Sudni kusini kwa kuwaunga mkono Waasi wa SPLM-N, lakini Sudani kusini imekuwa ikipinga shutma hizo.
 

Wachambuzi wa nchini Sudani wanasema mapigano ya Blue nile na Kurmuk si ya kushangaza kwa pande hizo mbili kwa kuwakila upande unataka kuonesha kuwa una nguvu kuliko mwingine wakati huu kabla ya Mazungumzo ambayo yanategemewa kufanyika kati ya Waasi na Serikali.
 

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika umetoa kipindi cha Miezi minne kwa Majeshi ya Waasi wa SPLM-N na Serikali kufikia makubaliano.