DR Congo

Watu 36 wapoteza maisha kufuatia mapigano kati ya Makundi ya Waasi nchini Congo

Mkuu wa Majeshi ya waaasi wa M23,Sultani Makenga
Mkuu wa Majeshi ya waaasi wa M23,Sultani Makenga REUTERS/James Akena

Mgawanyiko katika kundi la waasi la M23 Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo umesabisha mapigano makali kati ya waasi hao na kusababisha vifo vya watu 36 kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano haya yamezuka baada kiongozi wa kijeshi wa kundi la M 23 Sultan Makenga kumfuta kazi kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo Jean Marie Runiga kwa tuhma za kumhusisha Bosco Ntaganda.

Wakati mzozo huu ukiendelea hofu imeanza kutanda Mashariki mwa nchi hiyo na kwa sasa kati ya watu 3,000 na 4,000 wamekimbia makwao na wanajificha katika kambi la kijeshi la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Dr Congo, Joseph Kabila ameapa kuzidisha juhudi za kulinda usalama wa mashariki mwa nchi hiyo, wakati huu ambapo Mataifa ya jirani yametia saini Makubaliano ya kutoingilia maswala ya ndania ya nchi nyingine.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema katika Ripoti yake kuwa Mataifa ya kigeni bado yameendelea kuwaunga mkono Waasi wa Congo na kuwa watalipa kutokana na Vitendo hivyo.