DRC

Jeshi la serikali ya DRC laondoa vikosi vyake mjini Rutshuru

Wanajeshi wa serikali ya DRC
Wanajeshi wa serikali ya DRC news@yahoo.com

Jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC limeondoa vikosi vyake mjini Rutshuru mwishoni mwa juma siku moja tu baada ya kuudhibiti mji huo huko kaskazini mwa mji wa Goma, na hivyo kuwapa mwanya waasi wa M23 kuudhibiti upya mji huo. 

Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa Jeshi la serikali FARDC,wamesema walitii amri ya viongozi wa ngazi za juu huko Kinshasa,Jambo ambalo limeyahuzunisha mashirika ya kiraia katika jimbo la Kivu ya kaskazini.

Kwa upande wa kundi la M23,msemaji wakeBertrand Bisimwa amesema kuwa tayari walikuwa wamewapa wanajeshi hao wa serikali tahadhari kali kuwataka waondoke mara moja katika mji huo kwa muda usiozidi saa 2.

Hatua ya kuondoka kwa majeshi ya serikali huko Rutshuru imepokelewa kwa mshangao mkubwa kwa kile kinachoelezwa kuwa kuwepo kwa wanajeshi wa serikali mjini humo,ilikuwa ishara tosha kuhusu kurejea kwa utawala rasmi wa serikali katika eneo hilo lililokuwa chini ya udhibiti wa waasi wa 23.