Jengo kuu la usalama nchini Misri lachomwa moto
Jengo kuu la usalama mjini Port Said nchini Mirsi limechomwa moto jana Jumatatu huku mapigano yakizuka kati ya polisi na waandamanaji katika mji wa Suez Canal na kuua watu sita.
Imechapishwa:
Moto huo ulianza katika sakafu ya chini ya makao makuu ya jengo hilo na kueneza moshi mzito angani wakati vurugu zikiendelea katika mitaa kuzunguka jengo hilo.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa waokoaji hawakuweza kufika katika eneo la tukio, huku hasira za wananchi zikitajwa kuongezeka katika mji huo ambapo kampeni ya ukaidi dhidi ya serikali ikiingia wiki yake ya tatu.
Machafuko yanayoendelea nchini humo yamechochewa na adhabu ya kunyongwa hadi kufa waliyohukumiwa mashabiki wa soka nchini humo kwa kusababisha vurugu wakati wa mechi za kirafiki mwaka jana ambapo siku ya Jumapili vurugu hizo zilianza upya na kusababisha vifo vya watu sita ikiwa ni pamoja na askari polisi watatu.