MISRI

Mapigano mapya yazuka nchini Misri

Mapigano mapya yamejitokeza kati ya Polisi na Waandamanaji mjini Port Said,nchini Misri Mji ambao watu sita walipoteza maisha wakati wa mapambano mwishoni mwa juma.

Waandamanaji mjini Port Said
Waandamanaji mjini Port Said nytimes.com
Matangazo ya kibiashara

Ghasia zilipamba moto katika eneo la Jengo la Usalama, ambalo sakafu yake ya kwanza ilichomwa moto huku polisi nao wakitumia Gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.

Ghasia za mjini Port Said zilichochewa na hatua ya mahakama nchini Misri kuwahukumu adhabu ya kifo wapenzi wa Soka kwa shutma za kuwa vinara wa vurugu.

Mapigano mengine yalizuka jana karibu na viwanja vya Tahrir mjini Cairo kati ya Polisi na Waandamanaji waliokusanyika kwa ajili ya shughuli za mazishi ya Mwanaharakati aliyeuawa wakati wa maandamano mwezi Januari ambaye mwili wake ulichukua majuma kadhaa kuweza kuubaini.