DRC

Polisi yaimarisha usalama Mashariki mwa DRC baada ya kuondolewa kwa waasi wa M23

Jenerali Charles Bisengimana
Jenerali Charles Bisengimana skyscrapercity.com

Polisi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imesema usalama wa wananchi unaendelea kuimarishwa mashariki mwa nchi hiyo tangu kuondolewa kwa vikosi vya wapiganaji waasi wa M23 katika mji wa Goma jimboni Kivu ya Kaskazini. 

Matangazo ya kibiashara

Akiwa ziarani jijini humo Mkuu wa Polisi nchini Congo,jenerali Charles Bisengimana amesema licha ya kuimarika kwa usalama katika mji huo,polisi inakabiliwa na baadhi ya changamoto,zikiwemo ukosefu wa vifaa vya kazi.

Hayo yanajiri wakati Serikali ya jimbo la Kivu ya Kaskazini,imeunda tume ya watu watakaochunguza mauaji yaliyofanyika katika mji wa Kichanga,Mtaani Masisi wakati wa mapigano baina ya wapiganaji wa Mai Mai wa kundi la APCLS,na jeshi la serikali FARDC,ambapo inakisiwa kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa,huku kukiwa na migogoro ya kikabila baina ya watu wa kabila la Hunde na watu wanaozungumza Kinyarwanda.