SOMALIA-UN

Somalia yaondolewa vikwazo vya ununuzi wa silaha

Reuters/Tiksa Negeri

Baraza la usalama la umoja wa Mataifa UNSC limeondoa vikwazo vya biashara ya silaha dhidi ya Taifa la Somalia kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuweza kuisaidia Serikali ya Somalia katika kupambana na Wanamgambo wa Kiisalmu wanaokabiliana na serikali hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Nchi wanachama 15 wa Baraza la usalama kwa pamoja walipitisha azimio la kuruhusu silaha nyepesi kuuzwa kwa vikosi vya kijeshi nchini Somalia wakati huu ambapo wanapambana kuilinda Mamlaka ya Somalia dhidi ya kundi la wanamgambo la al Shabaab lenye uhusiano mtandao wa kigaidi duniani wa Al Qaeda.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahmoud aliyechukua madaraka ya nchi hiyo mwezi Septemba mwaka jana amekuwa akishinikiza Baraza la Usalama kuondoa vikwazo vya biashara ya Silaha kwa nchi hiyo.

Mohamud amepokea kwa mikono miwili hatua ya umoja wa Mataifa akisema kuwa inaashiria kuimarika kwa hali ya kisiasa nchini Somalia na kutasaidia wanajeshi wake ambao mara kadhaa wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa silaha pale wanapopambana wa wapiganaji wa Al Shabaab.