Afrika Kusini

Nelson Mandela arejea nyumbani baada ya hospitali kukamilisha uchunguzi wa afya yake

REUTERS/Jonathan Evans/File

Mjumbe wa amani ulimwenguni na kiongozi wa zamani wa afrika kusini Nelson Mandela ameruhusiwa kurejea nyumbani kwake akitokea hospitali alikokuwa akipatiwa matibabu na kufanyiwa uchunguzi wa kawaida toka jana jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Rais wa nchi hiyo amesema kiongozi huyo ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kukamilika kwa vipimo alivyokuwa akifanyiwa.

Nelson Madela mwenye umri wa miaka 94 miezi mitatu iliyopita alilazwa kwa siku 18 akikabiliwa na maradhi ya mapafu pamoja na matatizo katika kibofu chake cha mkojo.

Kwa muda mrefu sasa hali ya kiafya ya rais huyo mstaafu imekuwa ya wasiwasi huku swala la umri mkubwa likitajwa kuchagia kudhoofu kwake.