BURUNDI

Mazungumzo ya kisiasa kuanza leo nchini Burundi

Reuters / Alessandro Di Meo

Wadau wa siasa nchini Burundi wanaanza mazungumzo ya kisiasa nchini humo kuanzia leo jumatatu. Mazungumzo hayo yanafanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura na yanatarajiwa kuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wote wa Taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Wanasiasa wamepongeza umoja wa mataifa UN kwa kuandaa mazungumzo hayo ambayo yamependekezwa kwa muda mrefu na wanasiasa hususani viongozi wa upinzani.

Wanasiasa wa upinzani ambao wamekuwa uhamishoni na kurejea nchini humo siku za hivi karibuni ni miongoni mwa wajumbe wanaoshiriki mazungumzo hayo.

Mpaka wakati huu bado vyama vya upinzani vimeendelea kuhimiza umuhimu wa uwepo wa uhuru wa kweli katika uwanja wa siasa nchini humo.

Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza hatahudhuria mkutano huo kutokana na kuwa katika ziara rasmi nchini Ufaransa kuanzia leo.