DRC

Wachezaji na wajumbe wa soka nchini DRCongo wakwama kwenda Algeria baada ya kukosa stakabadhi

Wajumbe sita wa soka wa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC waliostahili kuandamana na timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20 wameshindwa kusafiri na timu hiyo kuelekea nchini Algeria katika mashindano ya chipukizi hao yanayotarajiwa kuanza jumamosi hii.

rfi
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinasema kuwa Maafisa hao pamoja na wachezaji wengine wawili wameshindwa kusafiri kutokana na kukosa stakabadhi za kusafiria.

Mbali na hayo wachezaji hao pamoja na kocha wao Baudouin Lofombo bado hawajapata marupurupu yao.

DRCongo inashiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo na imepangwa katika kundi moja na Gabon, Mali na Nigeria.