MALI

Kundi la Al-Qaeda ladai kuwa limemuua mateka wa Ufaransa

Kundi la Kigaidi la Al-Qaeda Kaskaizni mwa Afrika linasema limemuua mateka mmoja raia wa Ufaransa aliyekamatwa nchini humo mwaka 2011.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti kutoka Mauritania zinasema kuwa kundi hilo la Al-Qaeda lilimuua Philippe Verdon tarehe 10 mwezi Machi kwa kile wanachokisema ni kulipiza kisasi dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini Mali.

Serikali ya Ufaransa inasema kuwa inachunguza uhakika wa ripoti hiyo ya Al-Qaeda kubaini ikiwa kweli raia wake ameuliwa na magaidi hao.

Wanajeshi wa Ufaransa walivamia Mali mwezi Januari baada ya waasi wa Kiislamu kuuteka miji kadhaa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Philippe Verdon na Serge Lazarevic mwenzake walitekwa nyara katika mji wa Hombori mwaka 2011 walipokuwa nchini Mali katika shughuli za kibiashara.

Majeshi ya Ufaransa zaidi ya Elfu 4 ambao wako nchini Ufaransa wanatarajiwa kuanza kuondoka nchini huo kuanzia mwezi ujao kwa mujibu wa serikali ya Ufaransa.

Wakati uo huo,  nchi ya Ufaransa imeitaka serikali ya Mali kuhakikisha inawashughulikia wanajeshi wote wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kaskazini mwa nchi hiyo bila kujali ni mwanajeshi kutoka nchi gani.

Hivi karibuni mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Mali yalivituhumu vikosi vilivyoko nchini humo kwa kushiriki kukiuka haki za binadamu kwa kuwatesa mateka wa kiislamu inaowakamata.

Kauli ya Ufaransa imetolewa na waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo Laurent Fabius ambaye amemtaka rais Diancounda Traore kuhakikisha nchi yake inawakamata wanajeshi wote wanaotajwa kuhusika na vitendo hivyo.