DRCongo

Bosco Ntaganda aanza kuhesabu siku akiwa chini ya ulinzi huko The Hague

Generali Bosco Ntaganda, mtuhumiwa wa ICC
Generali Bosco Ntaganda, mtuhumiwa wa ICC © CPI

Mbabe wa kivita na mtuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita wa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bosco Ntaganda, jana Jumamosi ametumia siku yake ya kwanza akiwa chini ya ulizi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC huko The Hague Uholanzi , baada ya kujisalimisha kwenye ubalozi wa marekani mjini Kigali nchini Rwanda juma hili.

Matangazo ya kibiashara

Ntaganda ambaye ni mtuhumiwa wa kwanza kujisalimisha kwa hiari katika mahakama ya ICC anatuhumiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu kama mauaji, ubakaji na kuajiri watoto kwenye jeshi lakem,makosa anayodaiwa kuyatenda kipindi alipokuwa mbabe wa vita huko Mashariki mwa DRC .

Mbabe huyu wa kivita maarufu kama The Terminator, alijisalimisha katika ubalozi wa Marekani nchi Rwanda siku ya Jumatatu akitaka kufikishwa The Hague kukabiliana na mashtaka dhidi yake.