AFRIKA KUSINI

Hali ya Afya ya Rais wa Kwanza Mzalendo nchini Afrika Kusini Nelson Mandela yaendelea kuimarika akipatiwa matibabu

Rais wa Kwanza Mzalendo wa Nelson Mandela akiendelea kupatiwa matibabu
Rais wa Kwanza Mzalendo wa Nelson Mandela akiendelea kupatiwa matibabu Reuters

Serikali ya Afrika Kusini imeeleza hali ya afya ya Rais wa kwanza Mzalendo wa Taifa hilo anayefahamika kama Baba wa Taifa Nelson Mandela maarufu kama Madiba inaendelea vizuri na anaendelea kupata matibabu.

Matangazo ya kibiashara

Mandela ameendelea kusalia Hospital kwa kipindi cha siku tano akipatiwa matibabu kutoka kwa jopo la madaktari wanaopambana na maradhi ya nimonia yanayomsumbua Kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini.

Rais ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma imeeleza taarifa wanazoendelea kupatiwa na madaktari zinaleta matumaini kwa kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94 afya yake inaendelea kuimarika.

Ofisi ya Rais Zuma imesema kwa sasa tatizo la mapafu ambalo lilikuwa linachangia Mandela kushindwa kupumua vizuri limeshughulikiwa ipasavyo na ameanza klupumua yeye mwenyewe bila msaada wa mashine.

Rais Zuma amesema jopo la madaktari limeendelea kuwa karibu na Mandela ili kuhakikisha anapona haraka na hatimaye kurejea nyumbani kuungana na familia yake pamoja na kuendelea na shughuli zake za kawaida.

Kiongozi wa Afrika Kusini Zuma pia amewashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakiliweka jina la Mandela kwenye maombi yao akisema hiyo ni sehemu ambayo itasaidia kupona kwake haraka.

Rais Zuma pia ameshukuru hatua ya mataifa mbalimbali kutuma salamu zao za pole kwa Mandela na kumtakia apone haraka huku akitoa mfano wa Marekani ambapo Rais Barack Obama alituma salama kama hizo.

Siku ya jumapili makanisa mengi nchini Afrika Kusini yaliendesha misa za kumuombea Mandela aweze kupona haraka kutokana na kuendelea kupatiwa matibabu katika hospital tangu afikishwe juma lililopita.

Hii ni mara ya nne kwa Nelson Mandela kufikishwa Hospital kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambapo mfumo wa upumuaji ndiyo umekuwa sababu za yeye kujikuta akilazimika kupatiwa matibabu.