AFRIKA KUSINI

Afya ya Rais wa Kwanza Mzalendo nchini Afrika Kusini Nelson Mandela yazidi kuimarika baada ya kuwa Hospital kwa siku 7

Rais wa Kwanza Mzalendo nchini Afrika Kusini Nelson Mandela anayeendelea kupata matibabu akisumbuliwa na nimonia
Rais wa Kwanza Mzalendo nchini Afrika Kusini Nelson Mandela anayeendelea kupata matibabu akisumbuliwa na nimonia Trevor Samson/AFP

Serikali ya Afrika Kusini imetangaza hali ya afya ya Rais wa kwanza mzalendo Nelson Mandela maarufu kama Madiba inaendelea kuimarika baada ya kupatiwa matibabu kwa kipindi cha juma moja Hospitalini.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma imeeleza hali ya afya ya Kiongozi huyo wa zamani anayetambulika kama Baba wa Taifa imeendelea vizuri na huenda akaruhusiwa kurejea nyumbani siku chache zijazo.

Taarifa ya Ofisi ya Rais Zuma imeongeza hata Jopo la Madaktari wanaomtibu Mandela wamefurahishwa na maendeleo yanayoonekana tangu alazwe hospital hapo kwa karibu siku saba sasa.

Mandela alifikishwa hospital juma lililopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya nimoni na sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu kutoka kwa Jopo Maalma la Madaktari linalomuangalia kwa karibu.

Madakatari wanaomtibu Mzee Madiba wamesema hali yake inaridhisha tofauti kabisa na alipofikishwa Hospital tarehe 27 ya mwezi Machi mwaka huu ambapo alikuwa anapumia kwa tabu kutokana na kusumbuliwa na maradhi mapafu.

Ofisi ya Rais Zuma imeeleza Mzee Madiba ameweza kutembelewa na watu wa familia yake ambao wamepata nafasi ya kuongeza naye kitu ambacho kinadhihirisha kuimarika kwa afya ya Kiongozi huyo wa zamani.

Mandela mwenye umri wa miaka 94 licha ya kuendelea kupata matibabu na afya yake kuimarika lakini hakujatolewa maelezo yoyote na Ofisi ya Rais Zuma ya kwamba ataruhusiwa lini kutoka Hospital.

Hii ni mara ya nne kwa Baba wa Taifa la Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela Madiba kufikishwa Hospitali kwa matibabu ambapo mara ya mwisho alitumia siku moja Hospital kwa uchunguzi wa afya yake huku mwezi Desemba akilazimika kukaa kwa siku 18.