Misri

Hali ya utulivu yarejea nchini Misri baada ya machafuko ya kidini ya jana Jumapili

Mashambulizi ya kidini nchini Misri
Mashambulizi ya kidini nchini Misri

Hali ya utulivu imerejea karibu na kanisa la waumini wa madhehebu ya copte baada ya kushuhudiwa machafuko yaliogharimu maisha ya mtu mmoja huku watu 84 wakijeruhiwa wakati wa mazishi na raia mmoja muumini wa dini hiyo ya copte. Polisi wamemiminika kwa wingi karibu na kanisa la mtakatifu Marco ambako waumini wa madhehebu ya Copte walikuwa wamekusanyika.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi ya kurushiana mawe yameshuhudiwa usiku kucha kati ya raia ambao wengi ni wa kata ya Abbassiya ambako waumini wa madhehebu ya copte wameonekana kwa wingi katika majengo ya kanisa.

Waziri wa mambo ya ndani Mohamed Ibrahim alielekea usiku kwenye eneo la tukio huku Rais wa Misri Mohamed Morsi akilaani mashambulizi hayo na kukiri kuguswa na machafuko hayo yaliosabanisha mtu mmoja kufikwa na umauti kufuatia pande hizo mbili kupambana.

Ghasia hizi ni muendelezo wa mapigano yaliyozuka mwishoni mwa juma na kusababisha vifo vya waumini wa Kikristo wanne na muumini mmoja wa Kiislam kitendo ambacho kimemkera Rais Morsi na kutaka viongozi wa kidini kusaka suluhu ya tatizo hilo.

Rais Morsi amesema mapigano hayo yenye mrengo wa kidini yamekuwa yakimkera na kutaka wananchi kutoamini yamechangiwa kwa sababu Chama chake cha Muslim Brotherhood kinatawala nchi hiyo.

Wakristo wanne na Muislam mmoja waliuawa siku ya Ijumaa katika machafuko jijini Al-Khoussous, ambapo mashambulizi kati ya wa Waislam waliowengi na wa kristo yamekuwa yakishuhudiwa nchini Misri.