Congo Brazaville - PARIS

Rais wa Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso azuru jijini Paris

Rais Hollande akimpokea Denis Sassou Nguesso rais wa Congo Brazaville
Rais Hollande akimpokea Denis Sassou Nguesso rais wa Congo Brazaville REUTERS/Philippe Wojazer

Rais wa Congo Brazaville Denis Sassou Nguesso anafanya ziara ya kikazi ya siku tatu jijini Paria nchini Ufaransa ambapo atapokelewa Ikulu ya Elysee pamoja na wizara mbalimbali ikiwemo wizara ya mambo ya nje ya Ulinzi. Rais Nguesso atakutana na viongozi mbalimbali wa Ufaransa kabla ya kukutana na raia wa Congo waishio jijini Paris

Matangazo ya kibiashara

Hii itakuwa ni mara ya pili Denis Sassou Nguesso anakutana na rais Francois Hollande tangu kuchaguliwa kiongozi huyo wa Ufaransa. Hata hivyo viongozi hawa wawili walikutana jijini Kinshasa mwezi Octoba mwaka 2012, wakati wa mkutano wa nchi zinazo zungumza lugha ya kifaransa"Francophonie" bila hata hivyo kufurahiana.

Rais wa Congo alipata kuzungumza kwa muda wa robo saa ambapo Francois Hollande alimueleza kuwa vyombo vya sheria huenda vikafuata mkondo wake kama vitakavyo, kuhusu fedha haramu.

Tayari msako ulifanyika kwenye majengo ya Nyumba ya binti wa rais Nguesso jijini Paris, jambo ambalo lilipokelewa kuwa la kichochezi.

Sassou Nguesso alitaraji kujiosha mbele ya viongozi wa Paris katika kusimamia mzozo wa jamuhuri ya Afrika ya kati na kuvutiwa na watu wa ukanda wa maziwa makuu kuusuluhisha mzozo wa eneo hilo. Hata hivyo Sasou Nguesso anaonekana kuwa kwenye nafasi ya pili nyuma ya rais Museveni.

Na huko nchini jamuhuri ya Afrika ya kati tangu kuangushwa kwa utawala wa rais Francois Bozize, Kiongozi wa Tchad ndie inaonekana kuchukuwa nafasi, Tchad ambayo serikali ya Ufaransa inaikubali kufuatia majesho yake kujiunga huko nchini Mali.

Ziara hiyo ya Rais Nguesso nchini Ufaransa inakuja siku kumi tu baada ya ziara ya  Rais wa Chine Xi Jimping kuzuru jijini Brazaville ambako alikuwa na mazungumzo na viongozi wa taifa hilo, Denis Sasosu Nguesso ambae anapokelewa leo jijini Paris.

China imepiga hatuwa katika kuwekeza nchini Congo katika kipindi cha miaka kumi iliopita. hâta hivyo, inafahamika rami kwamba Ufaransa ndie mshirika wa kwanza wa kiuchumi wa Congo. mwaka 2011 msaada wake ulifikia Euro milioni 24.

Utawala wa Congo unakubali na kuheshimu msaada wa Ufaransa na kukubali kwamba serikali ya Paris imesaidia katika mpango wa kupigiwa debe wa kufutiwa madeni nchi masikini zenye mzigo mkubwa wa madeni, hali iliosadia nchi hiyo kufutiwa deni lake kubwa. Jamuhuri ya Congo ilikuwa inahesabiwa kuwa nchi ya kwanza duniani yenye mzigo mkubwa wa madeni.