JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-AFRIKA KUSINI

Wafanyabiashara wa silaha walikuwa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati siku mbili kabla ya kuagushwa kwa utawa wa rais Bozize

Wapiganaji wa muungano wa seleka katika mji wa Bangui March 26
Wapiganaji wa muungano wa seleka katika mji wa Bangui March 26 REUTERS/Alain Amontchi

Gazeti la Sunday Times la nchini Afrika Kusini limemuweka pabaya rais wawa nchi hiyo baada ya kuchapidha habari kuhusu uhusiano wa serikali yake na ule wa rais Francois Bozize ulioangushwa nchini jamuhuri ya Afrika ya kati.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na gazeti hilo, wafanyakazi wawili wa kiwanda kinachotengeneza silaha nchini Afrika kusini walikuwa mjini Bangui siku moja kabla ya mji mkuu wa jamuhuri ya Afrika ya kati kuanguka mikononi mwa waasi Machi 24.

Mmoja kati ya wafanyakazi hao wa kiwanda cha silaha Miles Chambers amelithibitishia gazeti hilo kwamba alikuwepo mjini Bangui machi 22 pamoja na mwenziye Clement Salanga pamoja na Emmanuel Rutman mshauri kutoka jijini Paris bila hata hivyo kujuwa kuhusu mpango wa kuipindua serikali ya rais Bozize.

Mwenyekiti wa kiwanda hicho kinachotengeneza silaha cha Paramount Ivor Ichikowitz amesema hapakuwepo na mkataba wowote kuhusu uuzaji wa silaha jijini Bangui, bali kulikuwa barua ya mualiko kutoka ikulu ya rais Bozize ili kwenda kutowa utambulisho na mambo yalikuwa kwenye hatuwa za kwanza.

Kiongozi huyo wa kiwanda hicho ametambulishw ana gazeti hilo la Sunday times kama mtu wa karibu sana na rais Jacob Zuma na viongozi wengine wakuu wa chama madarakani cha ANC.

Rais Zuma anakabiliwa na shinikizo tangu kuuawa kwa wanajeshi 13 wa Afrika Kusini nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati ambako walikuwa wamepelekwa huko kwa ajili ya ulinzi zaidi wa serikali Bozize ambayo hata hivyo ilikuwa kwenye hatuwa za mwisho.

Hili lilikuwa ni pigo kubwa kuwahi kutokea kwa jeshi la Afrika kusini tangu kumalizika kwa utawala wa kikaburu nchini Afrika Kusini mwaka 1994.