Sudani Kusini

Wanajeshi watano wa India wauawa nchini Sudani Kusini wakawa katika operesheni ya kulinda amani katika jimbo la Joglei

Ndege ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Joglei nchini Sudani Kusini
Ndege ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Joglei nchini Sudani Kusini

Wanajeshi wa tano kutoka nchini Idia walioko katika kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini wameuawa katika mtego wa kuvizia katika jimbo la Joglei.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter msemaji wa wizara ya mambo ya nje Syed Akbaruddin amesema kwamba wanajeshi watano wa kikosi cha kulinda amani cha MINUSS nchini Sudani Kusini wameuawa huku wengine wanne wakijeruhiwa katika mtego wa kuvizia wa waasi ambao hadi leo hawajambulika.

tukio hilo limetokea wakati walipokuwa katika msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa katika aneo na Joglei lililopo katikati mwa Sudani Kusini na ambalo limekuwa halina utulivu.

Msemaji huyo amesema nchi yake inaendesha harakati za kusafirisha maiti za waliopoteza maisha.

Jimbo la Joglei linkumbwa na matatizo ya uslama mdogo ambapo mapigano ya kikabila na mapigano ya waasi na jeshi la serikali tangu pale Sudani Kusini ilipojipatia uhuru wake Julay 9 mwaka 2011 baada ya makubaliano mwaka 2005 yalioshuhudia vita vya muda mrefu kati ya kusini na kaskazini (1983-2005 na kugharimu maisha ya watu takriban milioni mbili)

Mwezi Desemba 2011, kundi la watu efu nane wa kabila la Lou Nuer waliwauawa takriban watu mia sita wa kabila la Murle.

Eneo lenye kuwa hatari sana ni la Pibor ambako kuna ngime kuu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.

Kiongozi wa operesheni ya MINUSS Hilde Johson ametahadharisha kuhusu vurugu na ukosefu wa usalama katika eneo hilo. Amewatolea wito watu wa makabila ya Lou Nouer, Murle na Dinka, viongozi wao na uongozi wa jimbo la Joglei na serikali ya Sudani Kusini kuanzisha mchakato wa amani.