Kenya

Ma katibu 22 wa baraza la mawaziri kuteuliwa siku moja tu baada ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta

Uhuru Kenyatta na mtangulizi wake Mwai kibaki wakati wa sherehe za kuapishwa April 9
Uhuru Kenyatta na mtangulizi wake Mwai kibaki wakati wa sherehe za kuapishwa April 9 REUTERS/Thomas Mukoya

Rais mpya wa jamuhuru ya nne ya Kenya Uhuru Kenyatta na makam wake William Ruto, wanataraji kuwateuwa makatibu 22 wa baraza la mawaziri hii leo, kabla ya makatibu hao kupigwa msasa bungeni, lakini pia wananchi watashiriki katika kuwapiga msasa. Baraza hilo linatarajiwa kuwa na sura mpya.

Matangazo ya kibiashara

Awali walijulikana kama mawaziri na waliteuliwa moja kwa moja na rais lakini chini ya katiba mpya ya Kenya ilioidhinishwa mwaka 2010, sasa wataitwa makatibu wakuu wa wizara na watateuliwa na rais kisha kupigwa msasa bungeni kabla ya kuidhinishwa rasmi na kuapishwa kabla ya kuanza shughuli zao rasmi.

wananchi wa Kenya vilevile watashiriki katika sughuli za kuwapiga msasa. Kwa mujibu wa wataalamu ma maswala ya siasa, katika kuwateuwa makatibu hao 22, rais Uhuru Kenyata na naibu wake William Ruto lazima waafikiane baada ya kuketi pamoja na kutathimini majina ya makatibu waliopendekezwa.

Miongoni mwa walio pendekezwa katika orodha hiyo ya makatibu ni pamoja na Afisa mkuu mtendaji wa shirika  la  ndege la Kenya Titus Naikuni, afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Bidco Vimal Shah, aliekuwa mwenyekiti wa soko la hisa, Jimna Mbaru na mfanyibishara Easter Passaris miongoni mwa wengine .

Baraza hilo jipya linatarajia kuwa na idadi kubwa ya wanawake, ambapo jumla ya wanawake wanane watateuliwa, ikiwa ni pamoja na mshauri mkuu kwenye ikulu ya rais wa maswala ya siasa, Nancy Gitau, Mkuu wa Uongozi katika benki ya Kenya Anne Waiguru, katibu wa kudumu wa zamani katika wizara ya haki Amina Muhamed, kamishna wa zamani wa tume ya uchaguzi Winny Gachu, mbunge wa zamani wa katiani Wavinya Ndeti,  na naibu balozi wa Kenya nchini Somalia Ivoyne Khamati.

Wananchi wengi wa Kenya wanasubiri kuona jinsi ambavyo Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto watavyo shughulikia swala hilo.