DRCONGO-MONUSCO

Vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini DRCongo vimesema havitishwi na kampeni chafu za waasi wa M23

Vikosi vya MONUSCO
Vikosi vya MONUSCO

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinavyolinda amani nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO, vimesema kwamba haivitishwi na vitisho vinavyo tolewa na kundi la wapiganaji waasi wa M23 mashariki mwa jamuhuri ya Kidemokrasia ya DRCongo, ya kwamba watawashambulia wanajeshi wa kikosi maalum cha Umoja huo kitachotumwa hivi karibuni mashariki mwa DRCongo  kupambana na waasi.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Kinshasa, msemaji wa Monusco Manodje Mounoubai amesema kwamba hawatishiki na kampeni za uchochezi zinazo endeshwa na viongozi wa kundi hilo na kwamba wapo tayari kwa mapambano.

Waasi wa kundi la M23 wamekuwa wakitowa vitisho kwa majeshi ya Tanzania, Malawi na Afrika Kusini yanayo tarajiwa kuwa sehemu ya kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa UN kitachokuwa na jukumu la kupambana na makundi ya waasi wanaoyumbisha usalama mashariki mwa DRCongo.

Kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kitachopelekwa mashariki mwa DRCongo kinaendelea na maandalizi yake ambapo msemaji wa kikosi hicho felix Prosper Bass naye akadokeza kuwa mipango yote imekamilika na kwamba uchochezi wa kundi la waasi wa M23 dhidhi yao hauna maana yoyote.