GHANA

Wachimba migodi 16 wauawa nchini Ghana baada ya mgodi kuporomoka

Watu 16 wameuawa baada ya kuporomoka kwa mgodi wa dhahabu nchini Ghana.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wanasema kuwa hawana idadi kamili ya wachimba migodi waliokuwa ndani ya mgodi huo lakini wanaamini kuwa miili yote imeondolewa.

Ghana ni mojawapo ya nchi inayofahamika duniani kwa uchimbbaji wa dhahabu na zamani ilikuwa inafahamika kama Gold Coast kabla ya kupata uhuru mwaka wa1957 kutoka kwa Uingereza.

Serikali inasema wachimba migodi hao walikuwa haramu suala ambalo Accra inasema inaweka mikakati kushughulikia ongezeko la midogi haramu nchini humo.

Mwezi Machi mwaka huu raia 120 kutoka China walikamatwa nchini humo katika msako wa polisi wa kuwasaka wachimbaji haramu wa migodi ya dhahabu nchini humo.

Mwaka 2010 mgodi mwingine uliporomoka na kusababisha zaidi ya watu 100 kupoteza maisha.

Kwingineko, rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad anamalizia ziara yake ya siku tatu katika mataifa ya Afrika Magharibi nchini Ghana siku ya Jumatano na anakutana na rais John Dramani Mahama kuzungumzia uhusiano wa mataifa hayo mawili kidiplomsia na kibiashara.