SUDANI

Ban Ki Moon alaani mauaji ya askari wa kulinda amani jimboni Dahfur

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki-Moon amelaani mauaji ya askari mmoja wa kikosi cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika cha kulinda amani katika jimbo la Dahfur nchini Sudani.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa toka ofisi ya UN mjini Dahfur, Ban ametaka mamlaka nchini humo kuhakikisha wauaji wanakamatwa na wanafikishwa katika vyombo vya sheria.

Askari huyo aliuawa na wengine wawili walijeruhiwa baada ya kundi la watu kuvamia kituo chao kilichopo karibu na mji wa Muhagiriya.

Walinda amani zaidi ya 40 nchini Sudani wameuawa katika kipindi cha miaka mitano na miito mbalimbali imekuwa ikizidi kutolewa kwa wahusika wa mauaji hayo kuchukuliwa hatua za kisheria.