Cameroon

Rais wa Ufaransa ampongeza rais Paul Biya baada ya mateka saba wa Ufaransa kuachiwa huru

Rais wa Ufaransa Francois Hollande
Rais wa Ufaransa Francois Hollande REUTERS/Patrick Kovarik

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amemshukuru rais wa Cameroon Paul Biya kwa mchango wake katika kufanikisha kuachiwa huru kwa mateka saba wa familia moja raia wa Ufaransa ambao wamekuwa wakishikiliwa na wanamgambo wa Kiislam huko Magharibi mwa Africa kwa muda wa miezi miwili. 

Matangazo ya kibiashara

Biya, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 30 na alichaguliwa tena kwa muhula mwingine wa miaka saba mwezi Oktoba mwaka 2011 baada ya uchaguzi wa utata, kwa sasa anavuna thawabu ya kile alichokipanda wachambuzi wanasema.

Mateka hao waliwasili jijini Paris nchini Ufaransa mapema jana Jumamosi na kupokelewa na jamaa zao a rais Francois Hollande baada ya kuachiwa huru wakitokea Cameroon.

Hata hivyo serikali ya ufaransa haijaweka wazi ni kwa namna gani mateka hao wa familia ya Moulin-Fournier wameweza kuachiwa huru,zaidi ya kusema kuwa hakuna fidia yoyote iliyolipwa ili kuachiwa kwao na kwamba hakukuwa na operesheni za kijeshi kufanikisha hilo.