LIBYA

Serikali ya Ufaransa yaapa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waliotekeleza Shambulizi la Bomu

Shambulizi la Bomu nchini Libya dhidi ya ubalozi wa Ufaransa
Shambulizi la Bomu nchini Libya dhidi ya ubalozi wa Ufaransa Reuters

Serikali ya Ufaransa imeahidi wale ambao wamehusika na shambulizi la bomu la kujitoa muhanga lililotegwa kwenye gari katika Ubalozi wake huko nchini Libya watalipa kwa kile walichokifanya na wanauhakika watafanikiwa kuwakamata.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Laurent Fabius amezuru nchini Libya na kulitaja shambulizi hilo kuwa ni la kigaidi na kuwataka magaidi kutambua kwamba hawawezi kupambana na uwezo walionao kijeshi kukabiliana nao.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amekuwa ni miongoni mwa viongozi waliolaani shambulizi hilo na kutoa wito kwa Mamlaka nchini Libya kuhakikisha kuwa waliohusika kutekeleza shambulizi hilo wanafkikishwa mbele ya vyombo vya Sheria.

Shambulizi hilo limezua hofu ya usalama katika nchini ya Libya inayojipanga upya tangu kuangushwa kwa Utawala wa Kiongozi wao Marehemu Kanali Muamar Gaddafi baada ya Majeshi ya NATO kuwasaidia wapinzani kwenye mapigano hayo.

Hofu kubwa ya kutokana na kukosekana kwa usalama imetanda hasa katika maeneo ya kuzunguka mji wa Benghazi, eneo ambalo mashambulizi ya mabomu na mauaji yamewalazimu Raia kutoka nchi za Magharibi kuondoka.

Rai wanne wa Marekani akiwemo Balozi wa nchi hiyo nchini Libya Chris Stevens waliuawa mjini Beghazi baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana tarehe 11 mwezi Septemba.