Marekani

Baraza la Usalama kupitisha Azimio la kupeleka Vikosi vya kulinda amani nchini Mali

Vikosi vya Mali vilivyokuwa na Jukumu la kupambana na Wanamgambo nchini humo
Vikosi vya Mali vilivyokuwa na Jukumu la kupambana na Wanamgambo nchini humo France24 / capture d'écran

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, UN litapitisha Azimio hii leo la kuunda kikosi cha kulinda amani nchini Mali, kuchukua nafasi ya Majeshi ya Ufaransa na Vikosi vya Afrika nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho kitapelekwa nchini Mali ifikapo tarehe 1 mwezi Julai, kwa kipindi cha Miezi 12.
 

Jeshi la Mali lilifanya Mapinduzi mwezi March mwaka 2012 na kusababisha Ghasia ambazo zilitoa mwanya kwa Makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali kudhibiti sehemu kubwa ya nchi hiyo na kuweka utawala wa kiislamu.
 

Katika Ripoti iliyotoa pendekezo la kuundwa kwa Kikosi cha kulinda amani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema Operesheni ya Mali itakumbwa na Changamoto kubwa ikiwemo vitisho vya makundi ya kigaidi na Mbinu zao, usambazaji wa Silaha na milipuko.
 

Serikali ya Ufaransa imesema itawaacha takriban Wanajeshi 1,000 nchini Mali kati ya walio sasa 3,850 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
 

Kikosi cha kulinda amani nchini Mali kitakachofahamika kwa jina MINUSMA kitakuwa na Wanajeshi 11,200 na Polisi 1,440 Wakiwemo Wanajeshi wengine wa akiba watakaokuwa tayari kuingia nchini humo mara watakapohitajika.
 

Kikosi hicho kitaundwa kutoka Vikosi vya Afrika. Takriban Wanajeshi 6,300 nchi 10 za Jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi na Chad ambayo imepeleka vikosi vyake Mjini Bamako.
 

Kikosi kitakachoundwa hakitakuwa na jukumu la kupambana na Wanamgambo isipokuwa watakuwa wakilinda amani katika maeneo yenye Watu wengi hasa Kaskazini ili kuzuia Makundi ya Wanamgambo waliofurushwa kutorejea tena katika maeneo hayo.
 

Walinda amani watasaidia kufunza Wanajeshi wa Usalama wa nchini Mali pia watasaidia kuijenga upya Mali kwa kuandaa uchaguzi ulio huru, uwazi na haki wa Urais na Wabunge pia kuanza kwa ushirikishwaji katika Mazungumzo ya kitaifa na Mchakato wa Maridhiano.