Sudani

Marekani yatangaza kumpokea Mjumbe wa Somalia ili kujadili Mustakabali wa Amani ya Sudani

Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiiri
Rais wa Sudan Omary Bashir akiwa na rais wa Sudani Kusini Salva Kiiri UN Photo/Isaac Billy

Marekani iko tayari kumpokea Mjumbe wa juu kutoka nchini Sudan ikiwa ni harakati za kushawishi kutekelezwa kwa mpango wa amani wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Marekani ilialika ujumbe ukiongozwa na msaidizi wa Rais wa Sudan Omar al-Bashir, Nafie Ali Nafie baada ya kuonesha nia ya kusafiri mpaka Washington,Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan, Larry Andre ameeleza.
 

Andre amesema kuwa Tarehe ya ziara hiyo haijawekwa na kuwa Marekani imeiamia Sudan kuwa itatumia ziara hiyo kwa ajili ya kujadiliana juu ya mgogoro wa Sudani, maswala ya haki za binaadam na maswala mengine.
 

Mipango ya Ziara hii imekuja wakati ambapo kumekuwa na mwanga wa kuanza kwa Mazungumzo ya Amani yatakayofanyika nchini Ethiopia kati ya Serikali ya Sudan na Waasi wa SPLM-N ambao wamekuwa wakiendeleza uasi nchini humo.
 

Marekani imeendelea kuwa na Mawasiliano na Makundi ya Waasi na Nafie ameonekana kuwa na mchano mkubwa katika mazungumzo nchini Sudani.
 

Sudan ilitoa matumaini ya kuwa na Mahusiano mazuri na Marekani baada ya kuiruhusu Sudani kusini kujitenga mwaka 2011 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa Miongo kadhaa, hata hivykumekuwepo na mapiganno katika majimbo yanayotenganisha nchi hizo.
 

Wakazi wa Jimbo la Kordofani kusini na Blue Nile wanakabiliwa na njaa kutokana na Mashambulizi ya mabomu hivyo Wakazi hao kushindwa kuendelea na kazi za kilimo.