Afrika Kusini

Rais wa Afrika kusini Jackob Zuma atofautiana na Naibu wake kuhusu kupeleka tena Kikosi Jamuhuri ya Afrika ya Kati

Rais wa Afrika kusini, Jackob Zuma
Rais wa Afrika kusini, Jackob Zuma

Rais wa Afrika kusini na Naibu wake wametofautiana juu ya mpango wa kupeleka tena vikosi nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati ambapo Wanajeshi wake 13 waliuawa mwezi uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Rais Jacob Zuma amesema Mkutano wa jumuiaya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Kati (ECCAS) ambao alihudhuria nchini Chad umemuomba kupeleka tena Vikosi vyake.
 

Zuma amesema kuwa ombi hilo litafikiriwa baada ya kuwasilishwa rasmi, lakini wakati akihutubia Bunge nchini Afrika kusini, Makamu wake Kgalema Motlanthe ametofautiana na Rais Zuma akisema kuwa Serikali haina mpango wowote wa kupeleka Vikosi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
 

Wanajeshi 13 waliuawa nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati na wengine 27 walijeruhiwa tarehe 23 mwezi Machi baada ya kuwa katika mapambano na Waasi karibu na mji wa Bangui.
 

Tangu wakati huo Serikali ya Rais Zuma imekuwa ikihojiwa juu ya kwa nini Wanajeshi walipelekwa nchini humo, huku kukiwa na Shutma kuwa Wanajeshi hao walipelekwa kwa ajili ya kulinda maslahi binafsi.
 

Serikali imekana Shutuma hizo na kusema kuwa ilifuata taratibu zote za Bunge kabla ya Vikosi hivyo kupelekwa.