Mali

Baraza la Usalama laridhia kupeleka Vikosi vya kulinda amani nchini Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia kwa pamoja kupeleka Wanajeshi 12, 600 wa Kimataifa nchini Mali kuchukua jukumu la kulinda usalama kutoka kwa Vikosi vya Ufaransa na Afrika waliokuwa wakipambana na Wanamgambo wa kiislamu.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa unatarajia kupeleka vikosi kuanzia tarehe moja Julai, hata hivyo Baraza hilo litaangalia hali ya usalama kabla ya kuchukua hatua ya kufanya makabidhiano.

Mali ilitoa wito kwa Majeshi ya Ufaransa kuingia nchini humo mwezi Januari kupambana na Wanamgambo waliokuwa kwenuye hati hati ya kuingia jijini Bamako.

Majeshi ya Ufaransa na Vikosi vya Afrika yamefanikiwa kuwafurusha Wanamgambo kisha wakaelekea katika maeneo ya milimani na jangwani.

Ufaransa inamaliza Operesheni yake iliyohusisha Wanajeshi takriban 4,500 hata hivyo itaondoa sehemu ya Jeshi lake na kuacha Wanajeshi 1,000 nchini Mali ambao watakuwa na jukumu la kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Wanamgambo.

Azimio la Umoja wa Mataifa linasema Jeshi lifanye kila liwezekanalo kwa ajili ya kurejesha usalama wa Miji mikubwa, kulinda Raia na Kusaidia Serikali ya Mali kujiimarisha.