DRCONGO-M23

M23 Wafanya mkutano maalum, waliobakwa wahitaji msaada DRC

RFI

Wapiganaji waasi wa M23 wamekuwa na mkutano maalum mwishoni mwa juma lililopita mkutano ambao baadhi ya mashirika ya ujasusi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo yanasema utawapa mwanya waasi hao kujipanga juu ya namna ya kukabiliana na kikosi cha kimataifa kinacho tarajiwa kupelekwa eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na RFI-Kiswahili,msemaji wa Kundi hilo Rene Abandi amesema kuwa Kikao hicho ndicho kiliwafanya kuondoka Kampala kwa muda.

Hayo yanajiri wakati Vijana wa eneo la Rutshuru linalodhibitiwa na waasi hao wa M23 wamekuwa wakilalamikia kunyanyaswa na kukamatwa kwa nguvu kuingizwa jeshini,kama anavyosema hapa Sinzaera Wolff mkuu wa taasisi ya Vijana kwajili ya maendeleo mjini humo,

Wakati huohuo Shirika la wanawake kwa ajili ya maendeleo katika mji wa Goma limewatembelea wanawake zaidi ya 100 waliobakwa katika maeneo kadhaa ya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Mkuu wa Shirika hilo, Diane Kyambalo amesema lengo la ziara hiyo ilikua ni kuwafariji wanawake waliotendewa ukatili na watu kutoka makundi mbalimbali katika eneo la mashariki mwa DRCongo.

Kwa upande wake Bibi Sifa Shamavu ,mshauri wa wanawake waliobakwa na ambao wanatibiwa kunako Kituo cha Afya cha Heal Africa, anasema kuwa wanawake hao wanahitaji msaada zaidi,wa kiakili kwa kuwa wengi baadhi yao wanazidiwa

Shirika hilo limebaini kuwa Waathiriwa wa Ubakaji ni kutoka maeneo yenye kukumbwa na mapigano, na kwamba wengi baadhi yao wanateseka zaidi pale ambapo wanakataliwa na waume zao,kama anavyoeleza hapa mmoja wa wanawake hao.