MISRI

Mtoto wa kiongozi wa chama cha Muslim Brotherhood auwawa na watu wenye hasira

Kundi la wamisri wenye hasira wamemuua kiholela kijana mdogo wa kiongozi wa chama cha kiislamu cha Muslim Brotherhood, ambaye wanamtuhumu kusababisha mauaji ya mwanaume mmoja kufuatia kuandika maoni muhimu kuhusu harakati za chama hicho katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Face book. 

Wamisri wenye hasira wakishambulia nyumba ya wazazi wa  Yussef kabla ya kumkamata na kumwua
Wamisri wenye hasira wakishambulia nyumba ya wazazi wa Yussef kabla ya kumkamata na kumwua english.alarabiya.ne
Matangazo ya kibiashara

Vurugu zilizofanyika siku ya Alhamisi huko Nile Delta ni vurugu za karibuni katika mfululizo wa mauaji katika jimbo hilo huku ukiukwaji wa sheria ukizidi kushika kasi tangu kupinduliwa kwa rais wa zamani Hosni Mubarak.

Yussef Rabie Abdessalam, mwenye umri wa miaka 16 alifyatua risasi na kumwua mpita njia na kumjeruhi mmoja baada ya mabishano makali na mwanaume ambaye alikosoa wazi wazi chama cha Muslim Brotherhood kwa njia ya mtandao.