DRC

Waasi wa M23 waapa kupambana na vikosi vya kijeshi vya umoja wa mataifa UN

Wasiwasi umeendelea kuzingira hatima ya mazungumzo baina ya Waasi wa M23 na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC iwapo yataendelea kutokanana wajumbe wa pande zote kurejea nyumbani kipindi hiki Waasi wakiahidi watajibu mashambulizi iwapo Kikosi Maalum cha Umoja wa Mataifa kitashambulia ngome zake. 

Waasi wa M23
Waasi wa M23 rfi
Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo limesisitiza kuwa halitaki vikosi hivyo viingie nchini humo kutokana na kwamba vimepewa mamlaka ya kuwashambulia na hata kuwaua jambo ambalo halitaleta amani kama ambavyo jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanywa kuleta amani.

Tangu mazungumzo baina ya serikali ya Kinshasa na kundi hilo yarejerewe mwezi jana huko jijini Kampala nchini Uganda hakuna jipya ambalo limefanyika ambapo wadadisi wa mambo wanasema kuwa huenda mazungumzo hayo hayatarejerewa tena baada ya vikosi vya kijeshi kuanza kupelekwa Mashariki mwa DRC chini ya muungano wa umoja wa mataifa UN.

Kundi la M23 limesema serikali ya Kinshasa imesema kuwa haiko tayari kuendelea na mazungumzo hayo tena ingawa wao wanataka amani ya kudumu kwa mazungumzo na ikiwa hilo linashindikana nao watakuwa tayari kuvishambulia vikosi hivyo kwa risasi.